• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uber yaanzisha programu na kuwafanya madereza na wateja kuwa salama

    (GMT+08:00) 2018-07-13 19:04:06

    Kampuni ya kutoa huduma za usafiri wa texi nchini Kenya Uber imeanzisha programu ya kuweka siri namba za simu za madereva wake ikiwa ni mojawapo ya njia za kuwafanya wawe salama. Uber ilianzisha programu hiyo jana ikisema kwa muda mrefu madereva wake wamekuwa wakitatizwa na suala la usalama. Madereva watakuwa wakimpigia mteja simu bila namba zao kuonekana.

    Aidha Uber imeongeza kuwa maelezo zaidi kuhusu mteja yatakuwa yanajitokeza kwenye programu hiyo.Tangu mwaka wa 2016 Uber imekuwa ikivumbua programu mbali mbali zinazolenga kumfanya mteja na dereva kuwa salama kufuatia matukio mengi ya kiusalama kushuhudiwa kwa madereva wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako