• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vifo kutokana na shambulio la Bomu Kusini Magharibi ya Pakistan vimefikia 128

    (GMT+08:00) 2018-07-14 16:12:07

    Vifo kutokana na mlipuko wa kujitoa mhanga uliotekelezwa dhidi ya umati wa watu waliokuwa kwenye mkutano wa kampeni za kisiasa katika eneo la Mastung lililoko kwenye jimbo la Balochistan kusini Magharibi ya Pakistan vimeongezeka na kufikia 128.

    Akithibitisha vifo hivyo kaimu Waziri wa mambo ya ndani Agha Umar, amesema kufuatia mlipuko huo zaidi ya watu 120 wamejeruhiwa.

    Naibu Cammissioner wa mji wa Mastung Qiam Lashari amesema mlengwa hasa wa mlipuko huo alikuwa ni kiongozi wa kisiasa Nawabzada Siraj Raisani ambaye pia alihudhuria mkutano huo kwenye jimbo analoliongoza la Mastung.

    Kutokana na vifo hivyo, serikali ya jimbo la Balochistan imetangaza siku mbili za maombolezo. Na kupitia tovuti yake Kundi la kigaidi la Islamic State limetangaza kuwa ndilo lililotekeleza shambulizi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako