• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vikwazo vya usafirishaji wa silaha dhidi ya Sudan Kusini havisaidii kupatikana amani

    (GMT+08:00) 2018-07-14 16:12:25

    Balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Ma Zhaoxu amesema vikwazo vya usafirishaji wa silaha vilivyowekwa dhidi ya Sudan Kusini vinakwamisha mchakato wa kisiasa wa kutafuta suluhu ya mgogoro wa nchi hiyo.

    Balozi Ma, amelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kusikiliza maoni yanayotolewa na AU pamoja na IGAD kwamba matumizi ya hatua kali hazitasaidia kupata suluhu ya Sudan Kusini.

    Mchakato wa Kisiasa wa kutafuta suluhu ya mzozo wa Sudan Kusini umepata mafanikio chanya kutokana na maendeleo yake, jambo linaloonyesha kuwa amani itapatikana katika nchi hiyo na kwamba mzozo utamalizwa kwa njia za kisiasa.

    Aidha Balozi Ma, amesema China imekuwa ikiunga mkono mchakato wa amani ya Sudan Kusini na itaendelea kufanya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako