• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia yatarajia kurefusha makubaliano ya mafuta kwa bidhaa na Iran

    (GMT+08:00) 2018-07-14 16:28:35

    Waziri wa Nishati wa Russia Bw. Alexander Novak amesema nchi yake inatarajia kurefusha makubaliano ya kubadilishana mafuta kwa bidhaa na Iran, kwa kutumai kuwa Iran inaweza kununua bidhaa na huduma kutoka Russia, kupanua kiwango cha biashara ya nchi hizo mbili na kukuza maendeleo ya uhusiano wa nchi hizo mbili.

    Rais wa Marekani Donalad Trump alitangaza kuwa nchi yake itajiondoa kwenye mkataba wa nyuklia wa Iran na kuanzisha tena vikwazo kwa Iran. Vikwazo vinavyohusiana na mafuta ya Iran vitafanya kazi mwezi Novemba mwaka huu, vikilenga makampuni ya kigeni ambayo yanatumia mafuta kutoka Iran.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako