• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la usalama lalaani shambulizi la kigaidi nchini Pakistan

    (GMT+08:00) 2018-07-15 17:18:26

    Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa jana limetoa taarifa ya kulaani vikali shambulizi la kujitoa mhanga lililotokea kwenye mkoa wa Balochistan nchini Pakistan, vilevile baraza hilo limetoa salamu za pole kwa jamaa za watu waliofariki na kwa serikali ya Pakistan.

    Aidha, Baraza hilo limesisitiza kuwa ni lazima kuwaadhibu wahusika wa shambulizi hilo kwa mujibu wa sheria, pia limezitaka nchi nyingine zishirikiane na serikali ya Pakistan na pande nyingine zinazohusika , kutokana na sheria za kimataifa na majukumu yaliyowekwa na maazimio husika ya Baraza la usalama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako