• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakulima wa matunda wa Marekani wahofia athari za tofauti ya kibiashara kati ya Marekani na China

    (GMT+08:00) 2018-07-15 18:14:23

    Wakulima wa matunda katika jimbo la Kaskazini Magharibi nchini Marekani wameingiwa na wasiwasi kutokana na tofauti za kibiashara zilizojitokeza sasa baina ya Marekani na China baada ya ongezeko la ushuru kwa baadhi ya matunda kuongezeka tangu mwanzoni mwa mwezi huu.

    Wakulima wengi na wazalishaji wengi wamesikitishwa na athari za muda mrefu zinazotokana na msuguano wa kibiashara kati ya Marekani na China.

    Hata wakulima wa zao la mikaranga kutoka jimbo la Magharibi la Oregon la nchini Marekani, wameathirika kutokana na suala la ushuru na wameitaka serikali ya Rais Trump kufanya mazungumzo na China, ili kunusuru mapato yao kwenye soko la China.

    Naye mmoja wa wakulima wa Marekani Bw. Scott McIlrath ameeleza kuwa kupanda kwa ushuru kwenye usafirishaji wa matunda kutoka nchini Marekani kwenda China kutawalazimisha wakulima kuuza mazao yao kwenye soko la ndani.

    Aidha tofauti za kibiashara kati ya China na Marekani imekuja wakati mbaya kwa wakulima 1,400 wa zao la matunda damu (Cherries) kutoka jimbo la Washington, na wengine 1,100 kutoka maeneo tofauti ya Kaskazini Magharibi ambao kwa sasa wanavuna matunda hayo, ambayo inaelezwa kuwa China ni mnunuzi namba moja wa matunda hayo, hivyo suala la ongezeko la ushuru linahatarisha mapato yatokanayo na uuzaji wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako