• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNESCO yatumai kuimarisha uhusiano na China

    (GMT+08:00) 2018-07-16 09:13:26

    Katibu mkuu wa Shirika la Sayansi, elimu na Utamaduni la Umoja wa mataifa UNESCO Bibi Andrey Azoulaya amesema China inayounga mkono utaratibu wa pande nyingi ni mshirika wa kimkakati wa UNESCO, na UNESCO inapenda kuendeleza uhusiano kati yake na China ufikie kwenye ngazi mpya. Bibi Azoulaya anatarajiwa kufanya ziara ya kwanza nchini China kuanzia leo hadi Alhamisi tangu ateuliwe kuwa katibu mkuu wa UNESCO Novemba mwaka jana. Amesema dunia ya sasa inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo itikadi kali na suala la mabadiliko ya hali ya hewa, ambazo hakuna nchi yoyote inayoweza kuzikabili peke yake, na kwamba China ni nchi inayounga mkono utaratibu wa pande nyingi na mamlaka ya UNESCO, ambavyo ni muhimu katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako