• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Trump awasili Helsinki kwa ajili ya mkutano na Putin

    (GMT+08:00) 2018-07-16 09:43:57

    Rais Donald Trump wa Marekani jana jioni aliwasili Helsinki, nchini Finland kwa ajili ya mkutano na mwenzake wa Russia Vladimir Putin, ambao ni mara ya kwanza kwa viongozi hao kufanya mazungumzo ana kwa ana.

    Rais Trump aliwasili Helsinki moja kwa moja baada ya kumaliza ziara yake Scotland, na leo atafanya mazungumzo na rais Putin peke yao, na wanatarajiwa kukutana na wanahabari baada ya kumaliza mazungumzo.

    Mkutano kati yao utafanyika wakati kuna mvutano mkali kati ya Russia na nchi za magharibi kuhusu masuala ya Iran, Syria na Crimea, na mvutano kati ya Marekani na washirika wake wa NATO kuhusu biashara na ulinzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako