• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka: Ufaransa ndiyo mabingwa wa kombe la dunia 2018

    (GMT+08:00) 2018-07-16 10:45:06

    Timu ya taifa ya Ufaransa ndiyo mabingwa wa kombe la dunia kwa mwaka 2018 kutokana ushindi wa magoli 4-2 waliopata dhidi ya Croatia kwenye mechi ya fainali iliyopigwa jana mjini Moscow.

    Magoli ya Ufaransa kwenye mechi hiyo yalipatikana kupitia Antoine Griezmann, moja la kujifunga la Mario Mandzukic wa Croatia, Paul Pogba na jingine likifungwa na Kylian Mbappe, huku magoli ya kufutia machozi ya Croatia yakifungwa na Ivan Perisic pamoja na Mario Mandzukic.

    Kwa ushindi huo, timu ya taifa ya Ufaransa ilikabidhiwa kombe, medali za dhahabu pamoja na fedha taslimu dola za kimarekani milioni 38.

    Ufaransa inaingia kwenye rekodi ya kushinda ubingwa mara mbili ikiwa imewahi hivyo tena miaka 20 iliyopita mwaka 1998.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako