• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi wa China waongezeka kwa asilimia 6.8 katika nusu ya kwanza kwa mwaka huu

    (GMT+08:00) 2018-07-16 16:39:59

    Takwimu zilizotolewa tarehe 16 na Idara ya takwimu ya China zimesema kuwa, katika nusu ya kwanza mwaka huu, pato la taifa GDP limeongezeka kwa asilimia 6.8, uchumi wa China umedumisha mwelekeo wa kupata maendeleo yenye utulivu kwa hatua madhubuti. Msemaji wa Idara ya takwimu ya China amesema, katika nusu ya pili ya mwaka huu mwelekeo huo hautabadilika.

    Katika mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na Ofisi ya habari ya Baraza la serikali la China, msemaji wa Idara ya takwimu ya China Bw. Mao Shengyong amesema, katika nusu ya kwanza mwaka huu, uchumi wa China umedumisha mwelekeo wa kupata maendeleo . Anasema:

    "Kutokana na mahesabu ya awali, katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, pato la taifa GDP limefikia yuan trilioni 41.9, na hili ni ongezeko la asilimia 6.8. "

    Wakati huo huo, muundo wa viwanda, mahitaji, na biashara vyote vimeboreshwa. Bw. Mao Shengyong ameeleza kuwa, mazingira mazuri yanayosaidia uchumi kupata maendeleo yenye ubora wa juu yameimarishwa, hali ambayo imeweka msingi mzuri kwa ajili ya kutimiza malengo muhimu ya maendeleo katika uchumi na jamii kwa mwaka mzima, lakini wakati huo huo bado unahitaji kukabiliana na changamoto mbalimbali. Anasema:

    "Inapaswa kushikilia kufuata kanuni ya kufanya mageuzi ya kimuundo kwenye upande wa ugavi, kuendelea kupanua mahitaji yenye ufanisi, kufanya juhudi za kustawisha uchumi halisi (Real economy) kukabiliana changamoto kutoka nje, kuzuia na kukinga hatari na changamoto mbalimbali, ili kusukuma mbele ongezeko la uchumi, hatua za mageuzi, na kuboresha maisha ya watu ili kuhakikisha uchumi unadumisha maendeleo yenye utulivu kwa hatua madhubuti."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako