• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapeleka malalamiko ya ziada WTO kuhusu Marekani kuongeza ushuru kwa bidhaa za China

    (GMT+08:00) 2018-07-16 17:16:52

    Wizara ya biashara ya China imetoa taarifa kupitia tovuti yake ikisema, China imepeleka malalamiko ya ziada kwenye Shirika la Biashara Duniani (WTO) kuhusu pendekezo la Marekani la kutoza ushuru dhidi ya bidhaa za China zenye thamani ya dola bilioni 200 za kimarekani chini ya uchunguzi wa kipengele cha 301.

    Jumatano iliyopita, wizara hiyo ilisema China inapinga Marekani kutangaza orodha ya nyongeza ya ushuru kwa njia isiyo halali. Ili kulinda maslahi ya taifa na ya watu wake, serikali ya China itaendelea kuchukua hatua ya lazima kujibu kitendo hicho. Wizara hiyo hiyo imesisitiza kuwa, China inapinga kithabiti uonevu wa kibiashara wa Marekani na haina budi kulinda maslahi ya taifa na ya watu wake pamoja na biashara huria duniani na mfumo wa pande nyingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako