• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bei ya petroli kuongezeka wakati ya dizeli na mafuta taa kushuka

    (GMT+08:00) 2018-07-16 19:22:04
    Sasa utalipa Sh 3.39 zaidi kwa mafuta ya petroli kwa mwezi mmoja ujao hadi Agosti 14.

    Bei hizi mpya zimetolewa na Tume ya Udhibiti wa Nishati, bei ya mafuta taa na Dizeli bei zao zimeshuka Sh1.48 na Sh0.35 kwa mtiririko huo.

    Bei ya petroli Nairobi sasa ni Sh112.20, ya juu zaidi tangu Agosti 2014.

    Mafuta taa bei ya rejareja ni Sh85.73 wakati Dizeli ni Sh103.25.

    Mombasa mafuta ya petroli ni Sh108.90 mafuta ya taa Sh99.96 na dizeli Sh82.94.

    Bei ya mafuta imeongezeka kwa muda wa miezi 11 iliyopita baada ya kuongezeka kwa bei ya mafuta yasiyosafirishwa katika soko la kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako