• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa Marekani na Russia waanza mkutano wao wa kwanza wa pande mbili nchini Finland

    (GMT+08:00) 2018-07-16 20:31:41

    Rais Donald Trump wa Marekani na rais Vladmir Putin wa Russia wameanza mkutano wao wa kwanza wa pande mbili mjini Helsinki hii leo, na wanatarajiwa kujadili masuala mbalimbali.

    Akizungumza na waandishi wa habari, rais Putin amesema viongozi hao wamekuwa na mawasiliano ya mara kwa mara kwa njia ya simu na wamekutana katika matukio mbalimbali ya pande nyingi, na ni wakati wa majadiliano ya kina ya uhusiano wa pande mbili na masuala ya dharura ya kimataifa.

    Kwa upande wake, rais Trump amesema ataongelea masuala yanayohusiana na biashara, majeshi, makombora, na nyuklia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako