• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China akutana na mkuu wa Benki ya Dunia mjini Beijing

    (GMT+08:00) 2018-07-17 07:28:23

    Rais Xi Jinping wa China jana amekutana na mkuu wa Benki ya Dunia Bw. Jim Yong Kim mjini Beijing.

    Rais Xi amesema ushirikiano kati ya China na Benki ya Dunia unaendelea vizuri. China inaipongeza Benki ya Dunia kwa kuuunga mkono pendekezo la "Ukanda mmoja, Njia moja" pamoja na juhudi zake kwenye kuhimiza ongezeko la mitaji na mageuzi ya mfumo wa hisa katika miaka ya hivi karibuni, ambayo yamezisaidia nchi zinazoendelea ikiwemo China katika kuinua hadhi na haki ya kupiga kura.

    Rais Xi amesema Benki ya Dunia inafanya kazi muhimu katika kulinda utaratibu wa dunia yenye ncha nyingi na mafungamano ya kiuchumi. China inapenda kuimarisha uhusiano wa wenzi wa kimaendeleo na Benki ya Dunia, na kuendelea kulegeza masharti na kurahisisha biashara. China inapenda kushirikiana na Benki ya Dunia katika kuhimiza maendeleo endelevu na kupunguza umaskini, kulinda uchumi wa dunia ya ufunguaji mlango, na kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako