Shirika la Fedha la kimataifa IMF limedumisha makadirio ya ongezeko la uchumi kwa mwaka huu na mwaka kesho, lakini limetahadharisha kuhusu kuongezeka kwa mivutano ya biashara inayoweza kuuyumbisha ufufukaji wa uchumi wa dunia.
Kwenye ripoti iliyopitiwa upya kuhusu mwenendo wa uchumi wa dunia na kutolewa jana, IMF imesema mwaka huu na mwaka kesho ongezeko la uchumi wa dunia linatarajiwa kufikia asilimia 3.9, kama ilivyokadiriwa mwezi Aprili.
Hata hivyo IMF imesema makadirio hayo yanaweza kupungua kutokana na kuongezeka kwa mivutano ya kibiashara kati ya Marekani na washirika wake wa biashara. Ripoti imesema ushuru mpya uliotangazwa na Marekani na ushuru wa kulipiza kisasi uliotangazwa na washirika wake wa biashara umeongeza uwezekano wa kuongezeka kwa mivutano ya kibiashara.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |