• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Michezo, Kenya: Serikali yajiandaa kushinda medali nyingi katika Olimpiki 2020

    (GMT+08:00) 2018-07-17 10:14:53

    Waziri wa michezo wa Kenya Rashid Echesa amesema nchi yake sasa, ina matumaini ya kufanya vizuri kwenye mashindano ya Olimpiki ya mwaka 2020 nchini Japan, kutokana na maandalizi ya timu za vijana ikiwemo mafanikio yaliyopatikana kwenye mashindano ya dunia ya riadha kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 yaliyomalizika Julai 15 nchini Finland ambako huko Kenya walikuwa mabingwa kwa kutwa medali 11, zikiwemo 6 za dhahabu, 4 fedha na 1 ya shaba.

    Waziri huyo akisema kwa kushirikiana na chama cha riadha cha Kenya, serikali itahakikisha kutunza wanamichezo na kuwaandaa mapema kabla ya michuano hiyo ya olimpiki.

    Waziri Echesa alikuwa miongoni mwa maafisa waliosafiri na timu ya wanariadha waliokwenda kushiriki mashindano ya Finland.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako