• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Diego Maradona: Aanza majukumu ya uenyekiti wa klabu ya soka nchini Belarus

    (GMT+08:00) 2018-07-17 10:17:24

    Mchezaji wa zamani na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Argentina Diego Armando Maradona ameanza kutumikia wadhifa wake mpya kama Mwenyekiti wa klabu ya Dinamo Brest inayoshiriki ligi kuu ya nchini Belarus.

    Katika kuanza utekelezaji wa majukumu yake, Maradona alisaini baadhi ya mikataba ya maendeleo ya klabu ambayo kwa sasa inashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi.

    Maradona anajiunga na klabu hiyo baada ya kumaliza mkataba wa kuifundisha timu ya Al-Fujairah ya nchini Umoja wa Falme za Kiarabu, na tangazo kuwa atajiunga na Brest lilitolewa na klabu hiyo mapema mwezi Mei mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako