• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yakanusha lawama ya Marekani kuhusu China kutofuata kanuni za WTO

    (GMT+08:00) 2018-07-17 17:17:11

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amekanusha lawama zilizotolewa na Marekani kuwa China haifuatilii kanuni za Shirika la Biashara Duniani WTO.

    Hivi karibuni, Marekani imetoa ripoti kadhaa kulaumu China kutofuata kanuni za WTO na kuitumia kama kisingizio cha kutekeleza hatua ya biashara ya upande mmoja dhidi ya China.

    Bibi Hua amesema, China kufuata kanuni za WTO na kufanya juhudi kutimiza ahadi zake kwa Shirika hilo kunatambuliwa na jumuia ya kimataifa. Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Bw. Roberto Azevedo amesema, mchango uliotolewa na China kwenye shirika hilo unazidi kuongezeka siku hadi siku tangu ijiunge na shirika hilo mwaka 2001.

    Wakati huohuo, Bibi Hua akizungumzia mkutano wa viongozi wa Russia na Marekani amesema, China inafurahia kuona nchi hizo mbili kuboresha uhusiano kati yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako