• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Biashara mpya Afrika zimepokea dola milioni 160

    (GMT+08:00) 2018-07-17 20:13:06

    Wajasiriamali wanaoanza biuashara mpya barani Afrika hadi sasa wamepokea dola milioni 160 katika kipindi cha nusu ya kwanza ya 2018 wengi wakiwa ni kutoka nchini Kenya na Nigeria.

    Ripoti ya shirika la uchapishaji la WeeTracker inaonyesha kampuni tano mpya za Kenya ni miongoni mwa 10 zilizopokea fedha nyingi.

    Kampuni hizo ni pamoja na Cellulant, ilio na matawi katika nchi 11 iliopata dola milioni 47.5, M-Kopa dola milioni $10 na WeFarm dola milioni $5.

    Mkurungezi wa BootCamp Africa Zachariah George, amesema wengi wa wajasiriamali wa nchi kama vile Nigeria, Uganda, Ghana na Kenya wanapendelea biashara za mtandao, kilimo na teknolojia ya afya.

    Kulingana na ripoti hiyo ufadhilo wa sasa ni mara tatu ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako