• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wizara ya utalii kuunda Mamlaka ya Usimamizi wa Fukwe

    (GMT+08:00) 2018-07-17 20:13:59

    Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla amesema wapo katika mchakato wa kutunga sheria itakayounda Mamlaka ya Usimamizi wa Fukwe nchini ili kuweza kuzitumia bandari na fukwe kwa utalii.

    Aidha amesema wanakusudia kutafuta wawekezaji ndani na nje ya nchi ambao watasaidia kujenga bandari kwa ajili ya meli za kitalii ambazo zinatoka mataifa mbalimbali ziweze kuingia nchini.

    Akizungumza Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa nembo ya Urithi, Dk Kigwangalla amesema, baada ya sheria hiyo kukamilika itaweza kudhibiti bandari na fukwe kwa ajili ya utalii.

    Mkurugenzi wa Utalii, Deograsias Mdamu amesema, utalii una mchango mkubwa katika pato la Taifa na kwa mwaka 2017 watalii kutoka nje ambao waliingia nchini walikuwa ni milioni 1.3 na mapato ya dola za Marekani bilioni 2.3.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako