• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Miji kumi kunufaika na miradi ya maji Uganda

    (GMT+08:00) 2018-07-17 20:14:28

    Miji kumi nchini Uganda inatarajiwa kunufaika na miradi ya maji iliofadhiliwa na benki ya maendeleo barani Afrika.

    Benki hiyo imeidhinisha mkopo wa dola milioni 62 kufadhili miradi hiyo ya maji kunufaisha watu 390,000 kwenye miji 10.

    Lengo la serikali ni kuongeza upatikanaji wa maji safi katika miji mikubwa nchini humo ifikapo mwaka wa 2023.

    Wilaya zinazolengwa ni pamoja Kyenjojo, Nakasongola, Kayunga, Kamuli, Kapchorwa district, Dokolo, Bundibugyo na Buikwe.

    Mradi wote utagharimu dola milioni 69 na serikali ya Uganda itatoa kiasi cha dola milioni 6.9.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako