• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Trump hawezi kuokoa uhusiano kati ya Marekani na Russia bila ya kuacha mamlaka juu ya dola nyingine na hatua ya upande mmoja

    (GMT+08:00) 2018-07-17 21:15:58

    Rais Donald Trump wa Marekani na mwenzake wa Russia Vladimir Putin wamefanya mkutano rasmi kwa mara ya kwanza huko Helsinki.

    Masuala kadhaa yalizungumzwa kwenye mkutano huo ikiwemo uingiliaji wa Russia katika uchanguzi wa Marekani, suala la nyuklia la peninsula ya Korea, mapambano dhidi ya ugaidi, udhibiti wa silaha za nyuklia, pamoja na hali ya Iran na Syria.

    Ni wazi kuwa uhusiano kati ya Marekani na Russia ni mgumu sana, na migongano kati yao ni ya aina mbili, migongano ya maslahi na migongano ya msimamo wa thamani. Migongano ya maslahi inaweza kutatuliwa kupitia mazungumzo na maelewano, lakini migongano ya msimamo wa thamani haiwezi kutatuliwa ndani ya muda mfupi.

    Kutoamiana kwa nchi hizo mbili kunatawala uhusiano huo. Hali hiyo ilitokana na vita baridi, lakini haijatoweka kufuatia kumalizika kwa vita hivyo. Toka kumalizika kwa vita baridi hadi sasa, kushinikiza nafasi ya ushawishi ya Russia siku zote ni sera ya awamu zote za serikali ya Marekani. Hasa kufuatia Marekani kupanua mpaka wa Jumuiya ya NATO kwa upande wa Mashariki, rais Putin amebadilisha msimamo wake kwa Marekani na Jumuiya hiyo.

    Hivi sasa, ili kufufua uhusiano kati ya Marekani na Russia, licha ya kuvuka masuala magumu kama vile Ukraine, Syria na Iram, nchi hizo mbili pia zinatakiwa kukabiliana na hali ngumu ya kisiasa nchini Marekani katika uhusiano kwa Russia. Kama Marekani haiwezi kuacha mamlaka juu ya dola nyingine na hatua ya upande mmoja, mkutano wowote kati ya viongozi wa nchi hizo mbili utashindwa kuokoa uhusiano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako