• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa kuadhimisha Siku ya kimataifa ya Nelson Mandela

    (GMT+08:00) 2018-07-18 09:29:39

    Umoja wa Mataifa leo utafanya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Nelson Mandela kwa kuahidi kuendelea kupigania haki.

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema kwa njia ya video kuhusu maadhimisho ya siku hiyo, kuwa hayati Nelson Mandela alikuwa mtetezi wa kimataifa wa haki na usawa, ni nadra katika historia kuwa na mtu aliyefanya kazi nyingi kwa ajili ya kutimiza ndoto ya watu, na mapambano kwa ajili ya haki, heshima na usawa yataendelea.

    Tarehe 18 Julai kila mwaka ni siku ya kimataifa ya Nelson Mandela, iliyowekwa na Baraza kuu la Umoja wa Mataifa mwezi Novemba mwaka 2009, kwa ajili ya kutambua mchango wa Mandela kwa amani na uhuru.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako