• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Trump asema hataondoa vikwazo dhidi ya Russia

    (GMT+08:00) 2018-07-18 09:49:09

    Rais Donald Trump wa Marekani amesema, hataondoa vikwazo vilivyopo dhidi ya Russia na mazungumzo kati ya Marekani na Korea Kaskazini yataendelea.

    Akikutana na wabunge katika Ikulu ya Marekani, rais Trump amekanusha uwezekano wa kuondoa vikwazo dhidi ya Russia hasa baada ya kukutana na mwenzake wa Russia Vladimir Putin jumatatu mjini Helsinki. Pia amesema, rais Putin amekubaliana naye kuendelea na juhudi za pamoja za kuondoa silaha zote za nyuklia kwenye peninsula ya Korea. Ikulu ya Russia bado haijathibitisha habari hiyo.

    Kufuatia ukosoaji mkubwa kutoka kwa vyama viwili vya Marekani kwa kauli za kirafiki alizotoa kuhusu Rais wa Russia zilizoonekana kuungana na Rais huyu kuzishambulia idara za usalama za Marekani, Rais Trump alilazimika kuitisha mkutano na wabunge hao ili kufafanua kauli zake, na kusema ana imani kamili na kuyaunga mkono mashirika ya kijasusi ya Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako