• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda kuandaa Mashindano ya michezo kwa Shule za Afrika Mashariki mwaka huu

    (GMT+08:00) 2018-07-18 10:53:09

    Rwanda imethibitisha kuwa mwenyeji wa mashindano ya michezo kwa wanafunzi wa shule za kutoka Afrika Mashariki yatakayofanyika kuanzia Agosti 10 hadi Agosti 20 mwaka huu.

    Takribani wanamichezo 2600 wa timu 20 kutoka nchi za Uganda, Tanzania, Kenya na wenyeji Rwanda wanatarajiwa kushiriki, licha ya kuwa Burundi na Sudan Kusini zinaweza kuthibitisha kushiriki pia.

    Mashindano ya mwaka yatahusisha michezo 11 tofauti ambayo ni Mpira wa miguu, mpira wa wavu, mpira wa magongo, mpira wa pete, mpira wa kikapu, mpira wa mikono, raga, mchezo wa vinyoya, tennis, tennis ya meza, kuogelea na riadha.

    Katika hatua nyingine michezo ya mwaka huu itahusisha timu za shule ya msingi ambazo katika awamu hii ya kwanza ni wanamichezo 300 wamethitishwa kuwa watashiriki kutoka nchi za Kenya, Uganda na Rwanda, wakishiriki mpira wa miguu, mpira wa pete na mpira wa wavu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako