• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwanasoka Tim Cahill: Astaafu rasmi kuchezea timu ya Taifa

    (GMT+08:00) 2018-07-18 10:54:52

    Hatimaye mchezaji wa muda mrefu wa kimataifa wa Australia Tim Cahill ametangaza kustaafu kucheza katika timu ya taifa ya soka.

    Cahill mwenye miaka 38, anastaafu akiwa tayari ameandika rekodi kadhaa katika timu ya taifa, ikiwemo kuwa mfungaji bora wa wakati wote, kwa kuwa na magoli 50 katika mechi 107 alizowahi kucheza akiwa na Australia.

    Lingine la kujivunia kwa Cahill ni kuingia kwenye rekodi ya kushiriki mashindano ya kombe la dunia mara 4。

    Kupitia ujumbe alioandika kwenye mtandao wa Twitter, Cahill ameeleza kujivunia kutumikia nchi yake kwa miaka 14 tangu mwaka 2004.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako