• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka, Kombe la CAF: Yanga kucheza dhidi ya Gor Mahia leo mjini Nairobi

  (GMT+08:00) 2018-07-18 13:45:02

  Timu za kutoka Afrika Mashariki, Gor Mahia ya Kenya na Yanga ya Tanzania leo zinakutana katika mechi ya raundi ya tatu ya hatua ya makundi kwenye miichuano ya kombe la Shirikisho la soka Afrika kwa ngazi ya klabu.

  Gor ambao ni wenyeji katika mechi ya leo, wanashika nafasi ya pili kwenye kundi D wakiwa na pointi 2 baada ya kutoka sare katika mechi mbili zilizopita, lakini Yanga iko nafasi ya nne kwa kuwa na pointi moja kutokana na matokeo ya kufungwa mechi moja na kutoka sare mechi moja.

  Mechi nyingine ya kundi hili itafanyika leo mjini Kigali ambapo wenyeji Rayon Sport inayoshika nafasi ya tatu itawakaribisha USM Algiers ya Algeria ambayo inaongoza kundi hilo kwa kuwa na pointi 4.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako