• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UM wasifu uzoefu mzuri wa China katika kukinga na kuzuia kuenea kwa jangwa

    (GMT+08:00) 2018-07-18 16:42:04

    Mkutano wa mawaziri kuhusu maendeleo endelevu, utulivu na amani kwenye Baraza la ngazi ya juu kuhusu maendeleo endelevu la Umoja wa Mataifa umefanyika mjini New York, ambapo mjumbe wa China amefahamisha uzoefu wake kuhusu kukinga na kuzuia hali ya kuenea kuwa jangwa, na mfano wake mzuri wa "Jangwa la Kubuqi" umesifiwa na mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa na wawakilishi wa nchi mbalimbali.

    Katika mkutano huo, China ikiwa nchi mwenyekiti wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu kukinga na kushughulikia hali ya kuenea kwa jangwa, mjumbe wake alifahamisha uzoefu wa China uliopatikana katika kukinga na kushughulikia hali ya kuenea kwa jangwa. Mkurugenzi wa Idara ya misitu na malisho ya China Bw. Zhang Jianlong ameeleza kuwa, China ni moja kati ya nchi zenye maeneo makubwa zaidi ya jangwa, pamoja na idadi kubwa ya watu wanaoathiriwa vibaya zaidi na jangwa, na imepata mafanikio makubwa zaidi katika nyanja hiyo.

    Bw. Zhang Jianlong alifahamisha zaidi mfano wa "Jangwa la Kubuqi la mji wa Erdos" mkoani Mongolia ya Ndani wa China, kuhusu kupunguza hali ya kuenea kwa jangwa. Amesema mradi huo ulifanyika kupitia uungaji mkono wa kisera wa serikali, uwekezaji wa viwanda na kuwashirikisha wakulima na wafugaji kwenye masoko, kufanya uvumbuzi wa teknolojia, na kufanikiwa kupunguza jangwa kwa eneo la zaidi ya hekta laki 6, na kuwasaidia wakazi wa jangwa la Kubuqi na maeneo ya jirani zaidi ya laki 1 kuondokana na umaskini. Bw. Zhang Jianlong amesema, mafanikio hayo ni mfano mzuri wa ujenzi wa ikolojia nchini China, na pia ni kitambulisho cha ulinzi wa mazingira kinachotolewa na China kwa dunia nzima. Bw. Zhang Jianlong anasema:

    "Uzoefu uliopatikana kwenye Jangwa la Kubuqi unalingana sana na hali halisi iliyopo hivi sasa nchini China, ambayo imeshirikisha kwa pamoja na serikali, viwanda, jamii na wananchi wote. Kwa kweli mfano huo unaweza kutumiwa na nchi zote duniani hususan barani Afrika."

    Katibu mtendaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu kukinga na kushughulikia kuenea kwa jangwa Bibi Monique Barbut, amesema mfumo wa Jangwa la Kubuqi umeleta uwiano kati ya ikolojia, uchumi na maisha ya watu, ambao ni mfano mzuri unaofaa kuigwa na dunia nzima.

    "Mfano wa Jangwa la Kubuqi ni safi sana! Umetoa fursa za biashara katika hatua ya kurudisha ardhi kutoka jangwa. Huu ni mfano mpya biashara ya ikolojia unaojitokeza. Na tumejumuisha wajumbe wa nchi nyingi kujifunza uzoefu huo kutoka kwa China."

    Balozi wa kudumu wa Morocco kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Omar Hilale ameeleza kuwa, uzoefu wa China katika kukinga na kushughulikia hali ya kuenea kwa jangwa ukiwemo mfano wa Jangwa la Kubuqi, una umuhimu mkubwa sana kwa nchi za Afrika, na unatakiwa kuwa suala muhimu litakalofuatiliwa kwenye uhusiano wa ushirikiano na kiwenzi kati ya China na Afrika. Anasema:

    "Tunaikaribisha China kubadilishana uzoefu wake na nchi mbalimbali kuhusu kuzuia na kushughlikia hali ya kuenea kwa jangwa kwenye jukwaa la Umoja wa Mataifa. Mfano huo mzuri wa China umezitia moyo nchi nyingi duniani hususan nchi za Afrika. China na nchi za Afrika zina uhusiano imara wa kiwenzi, na kubadilisgana uzoefu katika nyanja hiyo unatakiwa kuwa suala muhimu kwenye uhusiano wa ushirikiano na kiwenzi kati ya pande hizo mbili."

    Bw. Zhang Jianlong pia ameeleza kuwa, katika siku za baadaye China itaongeza uwekezaji katika miradi inayohusika chini ya utaratibu wa ushirikiano wa kuzuia na kushughulikia hali ya kuenea kwa jangwa la "Ukanda mmoja, Njia moja", kuongeza uwekezaji katika miradi hiyo, utoaji wa msaada wa fedha kwa nchi mbalimbali zikiwemo Afrika, na kuandaa mafunzo kwa wataalamu wanaohusika ili kusukuma mbele ushirikiano kati ya kusini na kusini, na kutimiza utekelezaji wa lengo la kutokomeza hali ya kuenea kwa majangwa kwa misitu duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako