• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mbunge wa Marekani aihimiza serikali ya nchi hiyo kuacha kuongeza ushuru

    (GMT+08:00) 2018-07-18 17:14:07

    Mwenyekiti wa kamati ya fedha ya baraza la juu la bunge la Marekani inayoshughulikia usimamizi wa sera ya biashara, Bw. Orrin Hatch ameihimiza serikali ya nchi hiyo kuacha sera ya ushuru na kuanza kufanya mazungumzo na wenzi wa biashara, ikishindikana atawalishinikiza bunge kutunga sheria kuzuia mamlaka ya rais juu ya biashara.

    Akizungumza kwenye kikao cha baraza hilo, Bw. Hatch amesema, serikali ya nchi hiyo imetekeleza au kutishia kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 500 za kimarekani zinazoagizwa kutoka nje, na hatua hiyo itaweka familia na kampuni za Marekani kwenye hali ya hatari na kuharibu mafanikio yaliyopatikana kwenye mageuzi ya ushuru ya Marekani.

    Pia amesema, huu ni wakati wa kugeuka kwa mazungumzo ya kibiashara, na kuongeza kuwa hivi sasa anazungumza na wabunge wengine kuhusu machaguo husika ya utungaji wa sheria itakayoweza kuzuia mamlaka ya rais kuhusu biashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako