• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema vita vya kibiashara vilivyoanzishwa na Marekani ni dhidi ya dunia nzima

    (GMT+08:00) 2018-07-18 19:37:22

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying hapa Beijing amesema, vita ya kibiashara ilivyoanzishwa na Marekani sio tu inalenga China, bali pia ni dhidi ya dunia nzima, na imeweka uchumi wa dunia katika hali ya hatari.

    Bibi Hua amesema, vita hiyo ni kinyume na mwelekeo wa ukuaji wa uchumi wa dunia, na kuathiri imani na uchumi wa dunia, huku vikiharibu maslahi ya watu wa dunia nzima.

    Amesema vita hiyo imeleta wasiwasi ya jumuiya ya kimataifa, makundi makuu ya kiuchumi, mashirika ya kimataifa na kampuni za kimataifa zimeonesha ufuatiliaji mkubwa kwa vita hivyo.

    Wakati huohuo, Bi Hua Chunying ameipongeza serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC kwa kufanikiwa kudhibiti mlipuko wa Ebola mwezi Mei mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako