• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mamlaka ya mapato Tanzania kuongeza mapato kupitia sekta ya utalii

    (GMT+08:00) 2018-07-18 20:12:31

    Mamlaka ya mapato Tanzania ,TRA,imekuja na mkakati maalum wa kuhakikisha pato la serikali na kodi stahiki linapatikana kupitia sekta ya utalii nchini humo.

    Mkakati huo ni kushirikiana na taasisi zingine za serikali zilizopo kwenye sekta ya utalii zikiwamo Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa),Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Chama cha Wafanyabiashara wa Utalii (TATO) pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii na wadau wengine wanaojihusisha na utalii.

    Kamishna wa kodi za ndani Elijah Mwandumbya aliyasema hayo jana jijini Arusha na kueleza kuwa sekta ya utalii ni moja kati ya inayoiingizia serikali fedha nyingi za kigeni na hivyo inahitaji mkakati madhubuti ili kuongeza pato kwa serikali.

    Alisema kwa muda mrefu sekta ya utalii imekuwa ikifanya vizuri lakini bado inahitaji mkakati wa kuhakikisha kwamba kila pato linaloingia kupitia sekta hii inaongeza tija kwenye mapato ya nchi kupitia kodi mbalimbali kama zilivyoainishwa na sheria za kodi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako