• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yaingiza Sh188mn kutoka kodi ya mitandao ya kijamii na utumaji pesa kwa simu

    (GMT+08:00) 2018-07-18 20:12:56

    Uganda ilitangaza jumanne kuwa kufikia sasa imekusanya Ush7 bilioni (takriban Ksh188.4 milioni) kutoka kwa kodi mpya ya mitandao ya kijamii na miamala ya kutuma pesa kwa njia ya simu wiki moja tu katika mwaka mpya wa kifedha.

    Waziri wa Fedha David Bahati alisema ijapokuwa sbaraza la mawaziri liliidhinisha punguzo la ushuru katika miamala ya utumaji pesa kwa simu kutoka asilimia 1 hadi asilimia 0.5,punguzo hilo halitaathiri makadirio ya awali ya serikali ya kukusanya Ush118 bilioni (takriban Ksh3.2 billion) kutoka kwa kodi ambayo ilizua rabsha miongoni mwa umma.

    Bw Bahati alisema kuwa kikao cha jumatatu cha mawaziri kilifikia makubaliano kuwa kodi hiyo itozwe tu kwa utoaji wa pesa na sio utumaji.

    Kwa mujibu wa Waziri huyo ,takriban Ush11 trilioni zinatumwa katika majukwaa ya utumaji pesa ilhali Ush23 trilioni hutolewa kila mwezi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako