• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-Miradi zaidi kuvutia wawekezaji

    (GMT+08:00) 2018-07-18 20:13:26

    Zaidi ya miradi ya maendeleo 300 nchini inatarajiwa kuandikiwa andiko kwa lengo la kuwavutia wawekezaji wa ndani nan je ya nchi kuja kuwekeza.

    Hatua hiyo imefikiwa baada ya kuwapo kwa utangazaji zaidi wa mazingira mazuri ya uwezekaji yaliyopo nchini Tanzania kuliko utangazaji wa miradi ya maendeleo iliyopo.

    Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni inayohusika na ushauri wa biashara na mawasiliano ,Rodgers Mbaga,aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akielezea kuhusu maonyesho ya kukuza uwekezaji Tanzania (TIPEC),yanayotarajiwa kufanyika Novemba 14 hadi 16 mwaka huu.

    Mbaga alisema wanatambua nia ya serikali ya Rais John Magufuli ya kutangaza na kukuza uwekezaji ,hivyo wanaandaa maonyesho hayo ili kukuza miradi na kutafuta wawekezaji wenye mitaji.

    Alisema TIPEC itatambua na kuitengenezea andiko na kuitangaza miradi isiyoipungua 300 hususani inayohusu viwanda na kilimo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako