• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kombe la Shirikisho barani Afrika: Gor Mahia yatoa kipigo cha aibu kwa Yanga

    (GMT+08:00) 2018-07-19 08:31:06
    Yanga ya Tanzania imeshindwa kucheza muziki wa Gor Mahia fc ya Kenya katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuambulia kichapo cha mabao 4-0 mchezo huo uliopigwa jijini Nairobi usiku wa kuamkia leo.

    Ushindi huo wa Gor Mahia unawafanya waendelee kukalia nafasi ya pili katika kundi D wakifikisha jumla ya alama 5 huku MC Alger walio kileleni wakiwa na pointi 7 wakati Rayon Sports ya Rwanda ikishika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 2.

    Yanga imekuwa timu ya kwanza ndani ya kundi hilo kuruhusu mabao 9 baada ya kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya MC Algeria kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa huko Algeria.

    Mchezo mwingine: mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Thomas Ulimwengu, ameifungia bao la ushindi El Hilal ikiibwaga Songo ya Msumbiji magoli 2-1 katika mchezo wa Kundi B uwanja wa Al Hilal mjini Omdurman.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako