• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatetea hatua zake za kujibu ushuru wa Marekani dhidi ya chuma na Alumini

    (GMT+08:00) 2018-07-19 10:18:26

    Mkurugenzi wa kitengo cha sheria cha wizara ya biashara ya China amesema hatua za China za kujibu ushuru wa Marekani dhidi ya bidhaa za chuma na alumini ni halali, na zinaendana na kanuni ya biashara ya pande nyingi. Pia ameitaka Marekani isitishe hatua zake zinazokiuka kanuni za Shirika la biashara duniani WTO.

    Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa hatua ya Marekani ni ukiukaji mbaya wa kanuni ya biashara ya pande nyingi, na pia imehujumu maslahi halali ya nchi wanachama wa WTO ikiwemo China. Amesema China imelazimika kuchukua hatua kulinda maslahi yake halali, baada ya Marekani kukataa matakwa yake ya kufanya mazungumzo kuhusu suala la fidia.

    Wakati huo huo, Umoja wa Ulaya pia umetangaza kuchukua hatua ya muda ya kudhibiti gawio la bidhaa za chuma zinazoingizwa kutoka nje kuanzia leo, ili kuzuia bidhaa za chuma za nchi za nje zilizokusudiwa kuuzwa Marekani ziingie soko la Ulaya, kutokana na ushuru wa Marekani.

    Habari nyingine zinasema wizara ya biashara ya Marekani imetangaza kuanzisha uchunguzi dhidi ya uagizaji wa madini ya Uranium na bidhaa za Uranium kutoka nje, kwa mujibu wa kipengele cha 232 cha Sheria ya biashara ya Marekani, ili kujua kama uagizaji wa bidhaa hizo umetishia usalama wa Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako