• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yasema rais Trump aliomba kukutana na rais Rouhani

    (GMT+08:00) 2018-07-19 10:28:22

    Mkuu wa utumishi wa rais Bw. Mahmoud Vaezi amesema rais Hassan Rouhani wa Iran amepata maombi manane kutoka kwa mwenzake wa Marekani Donald Trump kwa ajili ya mkutano.

    Bw. Vaezi amesema maombi hayo ya rais Trump yaliyotolewa wakati rais Rouhani alipofanya ziara mjini New York kwa ajili ya kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwezi Septemba mwaka jana. Lakini hakusema kwa undani ni vipi rais Rouhani alijibu kuhusu mwaliko huo.

    Habari kutoka gazeti la Tehran Times zinasema Umoja wa Ulaya umeanzisha mfuko wenye dola za kimarekani bilioni 80 ili kutoa mkopo kwa makampuni madogo na yenye ukubwa wa kati katika kufanya biashara na Iran. Aliyekuwa katibu mkuu wa Baraza la Nchi Zinazouza Nje Gesi Bw. Mohammad-Houssein Adeli, amesema mamlaka za Ulaya zinapenda kupuuza vikwazo vya Marekani na kuzihamasisha nchi za Ulaya kufanya ushirikiano na Iran. Ameongeza kuwa kampuni za Iran pia zinaweza kuomba mikopo kutoka kwa mfuko huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako