• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Huenda kodi za mitandao ya jamii zikarekebishwa

    (GMT+08:00) 2018-07-19 20:33:58

    Serikali ya Uganda imeanza kuangalia upya kodi ya mitandao ya kijamii na huduma ya kutuma pesa kwa simu nchini humo.

    Hii ni baada ya malalamishi kwa wanaharakati na wabunge kutaka kodi hizo kupunguzwa.

    Hii ni baada ya maandamano kupinga kodi iliyoidhinishwa ya kutumia mitandao ya kijamii.

    Waziri wa habari na mawasiliano Uganda Frank Tumwebaze ametetea kuidhinishwa kwa kodi hiyo, akisema kwamba fedha zitakazopatikana zitatumiwa 'kuwekeza katika rasilmali zaidi za kimitandao'.

    Kodi hiyo ya shilingi 200 za Uganda ambayo ni sawa na dola za Marekani 0.05 inayotozwa ili mtu aweze kutumia mitandao kama Twitter na Facebook imechangia kuzuka maandamano nchini.

    Baadhi ya wabunge wanashinikiza kodi hiyo isitishwe kwa muda. Bunge litnatarajia kujadili hatua inayofuata wiki hii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako