• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjadala wa saba wa WTO kuhusu sera ya biashara na China wapata mafanikio

    (GMT+08:00) 2018-07-19 21:11:48

    Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng amesema, mjadala wa saba wa sera ya biashara wa Shirika la Biashara Duniani WTO na China uliofanywa hivi karibuni umemalizika huko Geneva na kupata mafanikio makubwa.

    Bw. Gao amesema, mjadala huo ni wa kawaida unaofanywa na WTO kwa nchi wanachama, na ulifuatiliwa na nchi wanachama wa shirika hilo. Kwenye mjadala, wanachama 70 walitoa hotuba, ambayo imeweka rekodi mpya kwenye ukaguzi wa shirika hilo.

    Pia amesema, kwenye mjadala nchi nyingi wanachama zimesifu mwelekeo wa sera na maendeleo yaliyopatikana nchini China na kupongeza mchango wa China na uongozi wake katika mfumo wa biashara wa pande nyingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako