• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashabiki wa Yanga wacharuka, wataka uongozi wa klabu kufanya maamuzi magumu

    (GMT+08:00) 2018-07-20 08:17:59
    Baada ya kupokea kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya Gor Mahia FC katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika, mashabiki wa Yanga wameutaka uongozi kukisafisha kikosi upya.

    Hatua hiyo imekuja kufuatia kipigo hicho cha aibu ugenini wakieleza kutoridhishwa na aina ya wachezaji wengi ilionao wakidai kuwa hawaendani na ukubwa wa kikosi cha Yanga.

    Tangu kuondoka kwa Kocha Mzambia, George Lwandamina, Yanga imekuwa ikiendelea na rekodi mbovu kutokana na kukosa matokeo chanya badala yake kikosi kimekuwa hakifanyi vema kama zamani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako