• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CECAFA Kombe la Challenge: Kilimanjaro Queens yaanza vibaya.

    (GMT+08:00) 2018-07-20 08:18:16
    Timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania Bara(Kilimanjaro Queens) imeanza vinaya michuano ya kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati baada ya kukubali kipigo cha goli 1-0 na wenyeji Timu ya Nyigu ya Rwanda, mchezo uliochezwa uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali jana.

    Bao pekee la Nyigu limefungwa na Alice Kalimba dakika ya 34 ya mchezo huo.

    Michuano hiyo iliyoanza jana nchini Rwanda, inashirikisha timu 5 za Afrika Mashariki. Katika mchezo wa utangulizi, timu ya taifa ya Uganda iliifunga timu ya taifa ya Kenya 1-0.

    Kesho Jumamosi Tanzania itamenyana na Kenya, huku Uganda itakutana na Ethiopia. Na Jumatatu Tanzania itamenyana na Uganda, wakati Rwanda watakutana na Ethiopia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako