FIBA imewafungia wachezaji 10 wa Ufilipino kutocheza michezo 35 huku wachezaji watatu wa Australia wakifungiwa jumla ya michezo tisa. Kocha wa Ufilipino Vincent Reyes amesimamishwa mchezo mmoja.
Vyama vya mchezo wa kikapu vya nchi zote pia vimetozwa faini na kuamriwa mchezo ujao wa nyumbani kucheza bila ya mashabiki.
Ugomvi huo katika robo ya tatu ya mchezo ambao Australia ilishinda kwa alama 89-53 ambapo wachezaji zaidi ya tisa wa timu mwenyeji waliingia uwanjani na kuzua ugomvi ambao ulichukua dakika 30 kuamuliwa kabla ya kuendelea tena.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |