• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNAIDS yaonya dhidi ya kupungua kwa kasi ya kuelekea lengo la Ukimwi

    (GMT+08:00) 2018-07-20 08:45:39

    Shirika la kupambana na ugonjwa wa Ukimwi la Umoja wa mataifa UNAIDS limeonya kuwa vifo vinavyotokana na Ukimwi havijapungua kwa kasi ya kutosha, na kutishia mafanikio ya kufikia malengo ya Ukimwi ifikapo mwaka 2020, ikiwa ni sehemu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa mataifa.

    Kwenye ripoti yake mpya, UNAIDS imesema idadi ya maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi kote duniani imeshuka kwa asilimia 18 katika miaka saba iliyopita, kutoka milioni 2.2 ya mwaka 2010 hadi kufikia milioni 1.8 ya mwaka jana, kasi ambayo haitoshi kutimiza lengo la kufikia chini ya laki tano kabla ya mwaka 2020.

    Ripoti pia imesema maambukizi mapya yameongezeka katika nchi 50 duniani, haswa katika Ulaya mashariki na Asia ya Kati, ambako idadi ya maambukizi mapya ya HIV kwa mwaka yameongezeka maradufu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako