• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Trump amtaka Bolton kumwalika Putin kwenda Washington mwishoni mwa mwaka

    (GMT+08:00) 2018-07-20 08:46:49

    Msemaji wa Ikulu ya Marekani Bibi Sarah Sanders amesema rais Donald Trump amemtaka mshauri wake wa usalama wa taifa Bw. John Bolton kumwalika mwenzake wa Russia Vladimir Putin mjini Washington katika majira ya mpukutiko mwaka huu.

    Kwenye ukurasa wake wa Twitter Bibi Sanders amesema huko Helsinki rais Trump amekubali kuendelea na mazungumzo ya kikazi kati ya mabaraza ya usalama ya nchi hizo mbili, na maandalizi ya kumwalika rais Putin yameanza.

    Rais Trump amekosolewa sana baada ya kukutana na rais Putin Julai 16 nchini Finland, kutokana na kauli zake zake ambazo wengi wanazichukulia kuwa ni alama ya ushirikiano na Russia dhidi ya shutuma zilizotolewa na mashirika ya intelijinsia ya Marekani, kuwa Russia iliingilia uchaguzi mkuu wa Marekani uliofanyika mwaka 2016.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako