• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Palestina yalaani Israel kupitisha sheria ya "nchi ya kiyahudi"

    (GMT+08:00) 2018-07-20 08:56:18

    Rais Mahmoud Abbas wa Palestina amelilaani bunge la Israel kupitisha sheria ya 'nchi ya kiyahudi' inayoitaja Israel kuwa ni nchi ya kiyahudi na mji mkuu wake ni Jerusalem. Amesema hakutakuwa na amani na usalama kama hadhi ya Jerusalem haitabaki kama ilivyo.

    Kwenye taarifa aliyotoa kupitia shirika la habari la Palestina WAFA, Bw. Abbas amesema sheria hiyo haitawakatisha tamaa wapalestina kwenye mapambano yao halali ya kushinda ukaliaji na kuanzisha nchi huru mpya.

    Umoja wa nchi za kiarabu jana pia ulililaani bunge la Israel kwa kupitisha sheria hiyo, na kusema sheria hiyo na nyingine zote zinazopitishwa kwa nguvu na Israel ni batili na haziwezi kuhalalisha ukaliaji.

    Sheria hiyo pia imeitangaza lugha ya kiebrania kuwa lugha rasmi na kuondoa kiarabu kama moja ya lugha rasmi za Israel.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako