• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa vyombo vya habari vya BRICS wafungwa

    (GMT+08:00) 2018-07-20 09:47:17

    Mkutano wa vyombo vya habari vya nchi za BRICS umefungwa jana baada ya wakuu wa mashirika makuu ya vyombo vya habari kukubaliana kuhusu mpango wa kuongeza ushirikiano kati yao katika mwaka huu hadi mwaka kesho.

    Kwa mujibu wa mpango huo, wakuu hao wamefikia makubaliano baada ya kubadilishana maoni kuhusu nafasi ya vyombo vya habari, majukumu ya kuimarisha uhusiano kati ya nchi za BRICS, kuongeza ushirikiano wa vyombo vya habari vya mtandao, na ushirikiano wa vyombo vya habari kati ya BRICS na nchi za Afrika.

    Washiriki wa mkutano huo wameona dunia inakabiliana na maendeleo, mageuzi na marekebisho makubwa kutokana na kuongezeka kwa hali za kutotabirika na mambo yanayoyumbisha utulivu na amani, lakini lengo kuu la kudumu la maendeleo ya binadamu ni kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja.

    Mkurugenzi mkuu wa idara ya biashara, viwanda na uwekezaji ya Afrika Kusini, Lerato Mataboge amesema, ingawa mafanikio makubwa yamepatikana kwenye nchi za BRICSkatika miaka 10 iliyopita, bado kuna nafasi kubwa ya kupata maendeleo zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako