• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa waonya dhidi ya kuongezeka kwa hatua za upande mmoja za kibiashara

    (GMT+08:00) 2018-07-20 10:02:23

    Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya kiuchumi na kijamii Bw. Liu Zhenmin ametahadharisha dhidi ya hatua zinazoongezeka za upande mmoja za kibiashara, ambazo anaona ni changamoto kwa mfumo wa biashara ya kimataifa.

    Bw. Liu amesema licha ya ukuaji wa uchumi, hatari kwa mustakbali wa uchumi zinaongezeka, na ametoa mwito wa kufanyika juhudi za kufufua uhusiano wa wenzi wa kimataifa kwa ajili ya maendeleo endelevu ili kujenga mfumo wa biashara ya kimataifa ulio jumuishi, wenye kanuni, uwazi na haki, na bila ubaguzi.

    Akizungumza katika mazungumzo ya kisiasa ya ngazi juu na taasisi za fedha za kimataifa yaliyofanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Bw. Liu amesema ukuaji mzuri wa uchumi hautoshi kuhakikisha mapato yanawanufaisha watu wengi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako