• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 14 wauawa kwenye shambulizi la anga kaskazini mwa Afghanistan

    (GMT+08:00) 2018-07-20 11:33:14

    Ofisa wa serikali ya mkoa Kunduz kaskazini mwa Afghanistan, amesema shambulizi la anga lilitokea jana mkoani humo limesababisha vifo vya watu 14.

    Msemaji wa serikali ya mkoa Kunduz amesema nyumba moja ya kiraia ilishambuliwa na kusababisha vifo vya raia 14 wakiwemo wanawake na watoto, na mmoja mwingine amejeruhiwa.

    Msemaji huyo amesema hajui kama shambulizi hilo lilifanywa na Jeshi la Marekani, lakini alisema serikali ya mkoa imetuma timu kufanya uchunguzi.

    Imefahamika kuwa shambulizi hilo lililotokea jana asubuhi huenda lililenga kituo cha kundi la Taliban kwenye eneo hilo, lakini hivi sasa haiwezi kuthibitishwa kuwa kama kuna wapiganaji wa Taliban miongoni mwa wahanga wa shambulizi.

    Kundi la Taliban limetoa taarifa kuwa shambulizi hilo lilifanywa na Jeshi la Marekani.

    Mpaka sasa Jeshi la Marekani nchini Afghanistan halijatoa maoni yoyote kuhusu taarifa hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako