• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vyombo vya habari vyatarajia kuimarisha ushirikiano na vyombo vya habari vya BRICS

    (GMT+08:00) 2018-07-20 17:11:21

    Wajumbe kutoka vyombo vya habari vya Afrika wanaohudhuria mkutano wa tatu wa vyombo vya habari vya BRICS unaofanyika huko Cape Town, Afrika Kusini, wamesema wanatarajia kuimarisha ushirikiano na vyombo vya habari vya nchi za BRICS ili kuripoti Afrika halisi.

    Mjumbe wa jarida la The Exchange la Tanzania Bw. Aly Ramji amesema, mazingira ya habari ya Afrika siku zote yanaongozwa na vyombo vya habari vya magharibi, hivyo vyombo vya habari vya nchi za BRICS vinaweza kuvisaidia vyombo vya habari vya Afrika kuimarisha ujenzi wa uwezo na kuripoti matukio halisi kwa mtazamo wa Afrika.

    Mjumbe kutoka gazeti la The Standard la Kenya Bw. Andrew Kangwa amesema, Afrika ina hadithi yake ya kusimulia kwa dunia, mafanikio yaliyopatikana katika nchi za Afrika pia yanatakiwa kuripotiwa kihalisi. Ana imani kuwa kupitia ushirikiano na vyombo vya habari vya nchi za BRICS, vyombo vya habari vya Afrika vitaweza kufanya vizuri zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako