• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema sera na hatua husika za Marekani zinatakiwa kulingana na wajibu wa msingi

    (GMT+08:00) 2018-07-20 19:47:55

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, Marekani, ikiwa nchi yenye nguvu zaidi duniani, sera na hatua zake husika zinatakiwa kulingana na wajibu wa msingi, na zinatakiwa kusadia kulinda utaratibu wa dunia badala ya kuuvuruga.

    Bi Hua amesema hayo baada ya mkurugenzi wa kamati ya biashara ya taifa ya Marekani Bw. Peter Navarro kusema kuwa, hivi sasa China inaleta hasara kwa nchi nyingine duniani katika sekta ya biashara, hivyo Marekani inatakiwa kushirikiana na nchi nyingine kukabiliana na hali hiyo.

    Bibi Hua amesema, China siku zote inatoa wito kuacha wazo la vita baridi, mamlaka juu ya dola nyingine na wazo la biashara linalonufaisha upande mmoja. Amesema lengo kuu la diplomasia ya China ni kuhimiza kujenga uhusiano wa kimataifa wa aina mpya wenye usawa na haki, unaoheshimiana na kunufaishana, na kuhimiza kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako