• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali yachukua hatua kuokoa sekta yha sukari

    (GMT+08:00) 2018-07-20 19:58:43

    Sekta ya sukari imekuwa ikikabiriwa na changamoto kadhaa ambazo zimeilazimu Serikali na wadau kuchukua hatua kila mara.

    Takwimu za Serikali zinaonyesha mahitaji ya sukari nchini Tanzania ni tani 630,000 kwa mwaka ambazo kati yake, tani 485,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na tani 145,000 ni malighafi viwandani.

    Licha ya kuwapo kwa wazalishaji wa ndani, wanaowashirikisha wakulima wadogo, uzalishaji bado hautoshi. Mabadiliko ya tabianchi na sababu nyinginezo bado zimeendelea kuwa kikwazo cha Tanzania kujitegemea kwa mahitaji yake ya bidhaa hiyo.

    Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema ukame uliozikumba nchi za ukanda wa mashariki, kati na kusini mwa Afrika mwaka 2017/18

    umesababisha Tanzania kushindwa kuzalisha tani 314,000 na kupata tani 300,399 pekee.

    Kutokana na upungufu huo, Serikali hutoa kibali cha kuagiza sukari kutoka nje.Aidha Mwijage amesema kampuni nne zinazozalisha sukari ndizo zilizopewa jukumu la kuagiza sukari kwa masharti kuwa hakutakuwa na upungufu wa sukari nchini humo na ni lazima wapanue mashamba ya miwa ili mpaka mwaka 2020 Tanzania ijitosheleze.

    Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango amesema ongezeko la ushuru wa forodha kwa asilimia 15 kutoka asilimia 25 mpaka asilimia 35 kwenye uingizaji wa sukari kwa lengo la kudhibiti upotevu wa mapato na kuhamasisha uzalishaji wa ndani.

    Kudhibiti uingizaji holela wa sukari, Serikali imesema ni kampuni nne pekee zitapewa la kufanya hivyo. Mwijage alizitaja kampuni hizo kuwa ni Kilombero, TPC, Kagera na Mtibwa. Licha ya kibali hicho, kampuni hizo ndizo wazalishaji wa sukari nchini.

    Haya yote yanafanyika baada ya Serikali kuendesha vita vya kukabiliana na magendo yaliyokuwa yanafanywa kwenye uingizaji na usambaji wa bidha hiyo nchini Tanzania na mataifa jirani yanayotumia Bandari ya Dar es Salaam.

    Pamoja na hayo, kuna ujenzi wa viwanda vingine vya sukari unaoendelea maeneo tofauti vinavyotarajiwa kuleta unafuu wa bei na kuongeza upatikanaji wa sukari nchini.

    Sukari ni bidhaa muhimu kwa matumizi ya nyumbani hata uzalishaji viwandani ingawa kwa miaka kadhaa ya nyuma kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa bidhaa hiyo na mfumuko wa bei.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako